Wabunge wasema viungo vya walemavu havitumiki kwenye chaguzi

0
363

Wabunge wameitaka jamii ya watu wenye ulemavu kuachana na dhana potofu ya kwamba viungo vya walemavu hutumiwa na wagombea wa nafasi mbalimbali katika harakati za uchaguzi ili kushinda nafasi wanazowania.

Wabunge wametoa rai hiyo katika uzinduzi wa kampeni ya Usiogope Tukopamoja inayoratibiwa na taasisi ya Sisi ni Sawa, inayopambana na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watu wenye Ualbino nchini.

Wamewataka walemavu kuondoa hofu na kushiriki katika shughuli za maendeleo bila wasiwasi wowote na kuhakikisha watoto wote wenye Ualbino wanapata haki ya elimu kama walivyo watoto wengine katika jamii

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Sisi ni Sawa, Henry Mdimu, amewaomba wabunge na wanasiasa nchini kutumia majukwaa ya siasa kutoa elimu kwa jamii dhidi ya dhana hiyo potofu.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambae pia ni balozi wa watu wenye Ualbino Mkoa wa Iringa, Mbunge Ritta Kabati amewasihi wabunge kuwa mabalozi katika kuhakikisha dhana hiyo inaondoka katika jamii.