Wabunge wapewa somo namna ya kuuliza maswali kwa Waziri Mkuu

0
138

Spika wa Bunge Job  Ndugai amewaambia Wabunge kuwa maswali yanayopaswa kuulizwa kwa Waziri Mkuu ni lazima yawe ya Kisekta ambayo pia yanatakiwa kufanyiwa utafiti.

https://www.youtube.com/watch?v=qaLi52oh0Zg&t=2s

Akihitimisha kipindi cha maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma, Spika Ndugai amewaambia Wabunge ni lazima wahakikishe maswali wanayomuuliza Waziri Mkuu yanakuwa ni ya kisekta ambayo hayahitaji majibu yenye takwimu.

Spika ndugai ameyakataa maswali mawili yaliyoulizwa katika kipindi hicho kutokana na kuwa nje ya kanuni ya maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu.

Maswali yaliyokataliwa ni la  Mbunge wa Babati Vijijini Jitu Soni lililohusu mkanganyiko wa ununuzi wa mazao na lingine la  Mbunge wa Temeke, – Abdalah Mtolea kuhusu tafsiri ya umri wa vijana.