Wabunge wanne wa ACT Wazalendo waapishwa

0
149

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, -Job Ndugai amesisitiza kuwa pamoja na uchache wa Wabunge kutoka upinzani, bado watapata haki ya kusikilizwa.

Spika Ndugai amesema hayo jijini Dodoma mara baada ya kuwaapisha Wabunge wanne kutoka Chama cha ACT Wazalendo, ambao wote wanatoka Visiwani Zanzibar.

Amewataka Wabunge hao kuendelea kuhubiri umoja na mshikamano wa Taifa ndani na nje ya Bunge.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mara baada ya kiapo hicho, Mbunge wa jimbo la  Konde, -Khatib Said Haji amesisitiza kuimarishwa kwa umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Hafla ya kuapishwa kwa Wabunge hao imehudhuriwa na wageni pamoja na viongozi mbalimbali.