Waathirika wa ukame Longido washikwa mkono

0
134

Rais wa Chama cha msalaba mwekundu Tanzania David Kihenzile ameshiriki zoezi la kugawa fedha na chakula lishe kwa Kaya zilizoathirika na ukame wilayani Longido Mkoani wa Arusha.

Kihenzile ambaye pia ni Mbunge wa Mufindi Kusini amewaeleza waathirika hao kwamba Redcross inatimiza jukumu la kuisaidia Serikali kutoa huduma za kibinadamu Nchini.

Hata hivyo ameishukuru serikali ya awamu ya sita kuwa karibu na TRCS na kuiwezeha kuwapatia msaada kaya 159 za jamii za kifugaji Wilayani Longido Mkoani Arusha ambapo kila Kaya imepata Shilingi 210,000.

Zoezi hilo lilianza mwezi machi mwaka huu ambapo wataalamu wa TRCS kupitia idara ya Maafa kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya sita walifanya tathmini ya waathirika wa Ukame na hatimaye kuungana na shirikisho la Red Cross Duniani kusaidia Kaya hizo ambapo kaya zaidi ya 400 zimenufaika kwa mikoa ya Arusha na Manyara.