“Tumezungumza masuala ya ulinzi na usalama na tukakubaliana vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viendelee kufanya kazi kwa pamoja ili tuhakikishe usalama kwenye nchi zetu, lakini pia kwenye ukanda wa Afrika Mashariki,” Rais Samia Suluhu Hassan akieleza aliyozungumza na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.