Vyombo vya habari vyatakiwa kutobagua Wasanii

0
172

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amevitaka vituo vya Televisheni na Redio nchini kuacha ubaguzi katika kucheza kazi za Wasanii.

Akizungumza mkoani Morogoro wakati wa mkutano ulioandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaoendelea mkoani Morogoro, Waziri Mkuu amevitaka vituo hivyo vya Televisheni na Redio nchini viwainue na kuwakuza Wasanii hao.

Amesema suala la kuamua kusikiliza au kutosililiza kazi za Wasanii liachwe kwa jamii, lakini vyombo vya habari visiwe na upendeleo ama ubaguzi.