Vunja Bei agawa vyombo kwa watumishi wa Mloganzila

0
206

Shija Kamanija maarufu Vunja Bei ametoa zawadi ya vyombo kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila).

Huu umekuwa ni mwendelezo wa zoezi lake la kugawa vyombo katika taasisi za serikali na leo wafanyakazi wa Hospitali ya Mloganzila wamejipatia zawadi hizo

Vunja Bei amesema anasikia fahari kutoa zawadi kwa watumishi na wafanyakazi mbalimbali kwa kuwa wanajituma sana kutimiza wajibu wao na kuunga juhudi za Rais Dkt. John Magufuli katika kuwatumikia Watanzania

“Mimi sio tajiri ila kwa sehemu tu kidogo ya faida yangu naamua kuwakumbuka watumishi wa Serikali ili kugawana nao faida katika biashara zangu,” Vunja Bei ameeleza.

Vunja Bei amekuwa akigawa zawadi ya vyombo katika taasisi za serikali hasa katika sekta ya elimu, afya na jeshi la polisi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.