Vuai, Mwinyi na Khalid wapenya tatu bora

0
392

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) kimepokea majina matatu ya wanachama wa chama hicho wanaowania Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Majina hayo ni Dkt Khalid Salim Mohamed, Dkt Hussein Mwinyi na Shamsi Vuai Nahodha.

Majina hayo ni kati ya majina matano yaliyochujwa ambayo ni Hamisi Musa Omar, Profesa Makame Mbarawa, Dkt Khalid Salim Mohamed, Dkt Hussein Mwinyi na Shamsi Vuai Nahodha.

Majina hayo matatu muda mfupi ujao yatapigiwa kura na wajumbe wa kikao hicho cha halmashauri kuu ya CCM ili lipatikane jina moja.