Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo amevitaka viwanda vinavyotumia vyuma chakavu kama malighafi, kujiepusha na ununuzi wa vyuma vinavyohujumiwa katika miradi mbalimbali.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 na kuongeza kuwa, hatua hiyo itasaidia kudhibiti wizi wa vyuma chakavu katika miundombinu ya miradi ya maendeleo.
Amesema vipo baadhi ya viwanda ambavyo vimekuwa vikiagiza vyuma chakavu bila kufuata sheria za mazingira, na pia havitumii fomu maalum ya kuonesha vimepokea vyuma chakavu kwa kiasi gani.