Viwanda vya MSD kuokoa Billioni 33

0
319

Kukamilika kwa ujenzi wa viwanda vya dawa hapa nchini vinavyojengwa na serikali kupitia bohari ya dawa nchini MSD kutasaidia kumaliza tatizo la upungufu wa dawa hapa nchini.

Hayo yameelezwa mkoani Njombe na Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali Watu kutoka bohari ya dawa nchini (MSD) Erick Mapunda, ambaye amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, serikali imejenga viwanda vitano vya dawa vinne mkoani Njombe na kimoja mkoani Dar es salaam ambavyo vinatarajiwa kuanza uzalishaji katika kipindi cha mwaka mpya wa fedha.

Viwanda hivyo vitasaidia kupunguza gharama za serikili za kuagiza dawa nje ya nchi ambapo shilingi bilioni 33 Kwa mwezi zilikuwa zinatumika katika kuagiza dawa kwenye mataifa ya nje.