Viwanda vya barakoa vyaanza uzalishaji

0
185

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai amesema Tanzania itaondokana na kuagiza barakoa nje ya nchi, baada ya kuanzisha viwanda vinavyotengeneza bidhaa hiyo.

Tukai ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kuhitimisha semina ya siku mbili kwa wahariri wa vyombo vya habari.

Amesema viwanda hivyo vitaisaidia Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kutokana na uwepo wa viwanda hivyo vya kutengeneza barakoa nchini, ambavyo tayari vimeanza uzalishaji.

Tukai amevitaja viwanda hivyo
vya kutengeneza barakoa kuwa ni cha Keko, Dar es Salaam ambacho kilianza uzalishaji mwezi Agosti mwaka 2020.

Amesema kiwanda kingine cha kutengeneza barakoa aina ya N-95 kilizinduliwa mwezi Machi mwaka huu katika ofisi za MSD Dar es Salaam.

Kuhusu kiwanda cha mipira ya mikono kilichopo Idodi, Makambako mkoani Njombe Mavere amesema, kinaendelea vizuri na kimetengeneza ajira zaidi ya 200 kwa Watanzania.

Amesema malighafi za kiwanda hicho cha kwanza Afrika Mashariki zinatoka Ifakara mkoani Morogoro na Lushoto mkoani Tanga.