Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Serikali kufanya kazi kwa nidhamu na bidii ili kusimamia maendeleo ya Taifa
Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Longido mkoani Arusha baada ya kuzindua mradi wa maji utakaowanufaisha zaidi ya wananchi elfu 13 huku mradi huo ukipeleka huduma ya maji hadi katika mji wa Namanga
Aidha Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakazi wa Longido kujitokeza kwa ajili ya zoezi la kuhesabiwa linalotarajia kufanyika mwakani nchini Tanzania