Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewaagiza Viongozi wa mkoa wa Kigoma kuhakikisha kero zote zilizoibuliwa wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani humo zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.
Makamu wa Rais ametoa agizo hilo wakati wa majumuisho ya ziara yake katika maeneo mbalimbali mkoani Kigoma, na kuwataka Viongozi hao kutenga siku maalum za kuwasikiliza Wananchi na kutatua kero zao.
Aidha, Dkt. Mpango amesema Serikali pamoja na mambo mengine imeweka kipaumbele katika sekta ya biashara, hivyo Viongozi wa mikoa yote nchini wana wajibu wa kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki kwa Wawekezaji.
Amemuagiza mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye kuitisha mkutano wa Baraza la Biashara la mkoa huo, ili kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara na kuzitafutia ufumbuzi.
Kuhusu migogoro baina ya Wananchi na askari katika maeneo ya hifadhi, Makamu wa Rais ameagiza uwepo ufumbuzi wa haraka katika maeneo hayo ili kuepusha hasara wanayopata Wananchi baada ya kufanya shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo na baadae kuzuiwa na mamlaka za uhifadhi.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Kigoma.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.