Viongozi wa SADC waendelea na mkutano wao

0
311

Rais John Magufuli amesema kuwa, Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zote Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kuhakikisha malengo ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo yanaendelea kuzingatiwa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nchi Wanachama wa SADC.

Amesisitiza kuwa, nchi za SADC pia zitahakikisha ndoto na mawazo ya Waasisi wa Jumuiya hiyo akiwemo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanaendelea kutekelezwa kwa vitendo na kurithishwa kwa vizazi vijavyo.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa SADC,- Stergomena Tax amesema kuwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi za Jumuiya hiyo zinazofanya vizuri katika kukidhi vigezo vya uchumi mpana na ambazo zimeweza kukuza uchumi wake kwa haraka.

Viongozi hao wa SADC wanakutana kwa muda wa siku Mbili, kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Jumuiya hiyo.