Viongozi wa dini watakiwa kusimamia maadili kwa vijana

0
169

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ameishukuru Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya kwa kuendelea kuiunga mkono serikali.

Amesema serikali inatambua mchango wa jumuiya hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali za wananchi hasa katika sekta ya afya, elimu, maji na nishati ya umeme.

Dkt. Mpango ametoa shukrani hizo mkoani Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya nchini Tanzania, wakiongozwa na kaimu Amiri wa Jumuiya hiyo Sheikh Abdulrahaman Ame.

Ameiomba jumuiya hiyo pamoja na viongozi wengine wa dini kuweka mkazo katika kusimamia maadili hasa kwa vijana kutokana athari zitokanazo na mitandao ya kijamii.

Makamu wa Rais amesema dini zinapaswa kuwa chanzo cha upendo na umoja baina ya watanzania, na hazipaswi kutumika kama chanzo cha chuki baina ya waumin