Viongozi wa Dini wataja sababu za kumuunga mkono Rais Magufuli

0
214

Askofu Zachary Kakobe amesema viongozi wa dini wameamua kuchagua upande kwa sababu Rais Magufuli amegusa dini kwa kiasi kikubwa sana.

Akitaja baadhi ya mambo aliyoyafanya amesema kuwa Tanzania imefungua ubalozi nchini Israel na nchini hiyo ina muwakilishi Tanzania, na kuwa uhusiano kati ya Israel na Wakristo ni kitu cha muhimu sana.

Ameongeza kuwa, kwa miaka mingi sana wamekuwa wakiomba uchaguzi mkuu usifanyike siku za ibada, lakini haikufanikiwa hadi Rais Magufuli alipoingia madarakani na sasa uchaguzi utafanyika siku ya Jumatano.

Amesema pia, Rais Magufuli alikataa kufunga nyumba za ibada wakati wa janga la virusi vya corona, jambo lililowapa faraja sana. Lakini pia amekuwa akihusika kwenye shughuli zote bila kujadili dili wala dhehebu.