Viongozi wa dini waombwa kuihamasisha jamii kushiriki kwenye uchaguzi

0
277

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, – Paul Makonda amewaomba Viongozi wa dini kuwahamasisha waumini wao kujitokeza katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwachagua Viongozi watakaowaletea maendeleo.

Makonda ametoa ombi hilo jijini Dar es salaam wakati wa Kongamano maalum kuelekea uchaguzi, uchumi wa viwanda, amani, mahusiano, uzalendo na ustawi wa jamii.

Uchaguzi huo wa Viongozi wa Serikali za Mitaa utafanyika Novemba 24 mwaka huu.