Viongozi wa CCM wametakiwa kushirikiana kwa karibu na serikali

0
256

Mwandishi Doreen Mlay

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi – CCM wametakiwa kushirikiana kwa karibu na serikali katika kusimamia maendeleo nchi.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt. John Magufuli wakati wa kikao cha viongozi watendaji wa Chama na Jumuiya zake za mikoa na wilaya.

Msisitizo zaidi ukawekwa kwa viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya shina kuangalia utekelezaji wa miradi inayofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa CCM kikao hicho kimehudhuriwa na watu elfu moja mia saba na themanini na idadi iliyokusudiwa ilikuwa elfu moja na mia nane.