Viongozi Tisa wa CHADEMA wakutwa na kesi ya kujibu

0
180

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imewakuta na kesi ya kujibu viongozi Tisa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, -Freeman Mbowe.

Mbowe na viongozi wengine Nane, wakiwemo Wabunge Sita wanakabiliwa na kesi ya jinai yenye mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi.

Uamuzi huo umetolewa hii leo na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo ya Kisutu, -Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao.

Washtakiwa wengine ni Mbunge wa Tarime Mjini,- Esther Matiko, Mbunge wa Iringa Mjini, -Mchungaji Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa kwa upande wa Zanzibar, – Salum Mwalimu na Mbunge wa Kibamba, -John Mnyika

Wengine ni Mbunge wa Kawe, -Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, – John Heche, Mbunge wa Bunda Mjini, -Ester Bulaya na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Vicent Mashinji.