Viongozi mbalimbali wateuliwa na Rais

0
166

Rais Samia Suluhu Hassan  amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, ambapo amemteua Mhandisi Bashir Mrindoko kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO).
 
Mhandisi MRINDOKO ni Katibu Mkuu Mstaafu.
 
Profesa Shabani Chamshama ameteuliwa 
kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF).
 
Profesa Chamshama ni Profesa wa Sayansi ya Misitu na Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Morogoro.
 
Rais Samia Suluhu Hassan pia amemteua Sarah Barahomoka kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Promotion of Rural Initiatives and Development Enterprises Limited (PRIDE).
 
Barahomoka ni Mwandishi Mkuu wa Sheria Mstaafu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Katika uteuzi huo Paul Sangawe  ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Self Microfinance (Self -MF).
 
SANGAWE ni Mkurugenzi wa Sera na Utaratibu wa shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma.
 
Dkt. Oswald Masebo  ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa (NMT).

 Dkt. MASEBO ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 
Rais amemteua Profesa Emmanuel Mjema kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Prof. Mjema ni Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dar es Salaam.

Tuma Abdallah  ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) na kabla ya uteuzi huo alikuwa akikaimu nafasi hiyo
 
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, IKULU uteuzi huo unaanza mara moja.