Viongozi mbalimbali wahani msiba wa Nelson Mabeyo

0
167

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo Msasani jijini Dar es salaam, kufuatia msiba wa mtoto wake Nelson Mabeyo.

Nelson alifariki Duniani hapo jana baada ya ndege ndogo aliyokua akiiendesha mali ya kampuni ya Auric Air, kuanguka muda mfupi baada ya kupaa katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera wilayani Serengeti mkoani Mara.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, akisaini kitabu cha maombelezo kwenye msiba wa mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, -Nelson Mabeyo, alipofika nyumbani kwa Mkuu huyo wa Majeshi jijini Dar es salaam.