Vilabu Afrika kuanza kupambana Septemba 10

0
189

Shirikisho ya Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), limetangaza ratiba ya kwanza ya mashindano ya vilabu barani Afrika kwa msimu wa 2021/2022.

Mashindano hayo yataanza rasmi kwa hatua ya awali Septemba 10 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba ya CAF, droo ya nani atakutana na nani katika raundi za awali itafanyika Agosti 15 mwaka huu.

Dirisha la mataifa kuomba kuandaa fainali za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho litafunguliwa mwezi Novemba mwaka huu, na katika michuano ya msimu wa 2021/2022 Tanzania itawakilishwa na Azam FC na Biashara United
kwenye Kombe la Shirikisho.

Simba SC na Yanga SC zenyewe zitangia kwenye Ligi ya Mabingwa 2021/2022.