Manispaa ya Kigoma – Ujiji, imekabidhi mkopo wa Shillingi Milioni 170 kwa vikundi 46 vya Wanawake, Vijana na watu Wenye ulemavu, ukiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi ya Serikali katika kuwainua Wananchi Kiuchumi.
Akikabidhi mkopo huo, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu, – Emmanuel Maganga amewataka Wanachama wa vikundi hivyo kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Pia amewataka kuhakikisha wanaendeleza kwa umakini shughuli zao za uzalishaji Mali ili waweze kukuza vipato vyao na hatimaye kurejesha mkopo huo.