Vijana wote waripoti TCU kupata utaratibu

0
184

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasisitiza Wanafunzi waliorudi nchini kutoka masomoni nje ya nchi kutokana vita vya Russia na Ukraine ama janga la UVIKO – 19 kuripoti Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili waelekezwe utaratibu utakaowawezesha kuendelea na masomo yao wakiwa Tanzania na kupata mwongozo wa kozi walizokuwa wanasoma.

“Tulitoa tangazo kupitia wizara vijana wote waripoti wizara ya elimu waende wakieleza walikuwa wanasoma kozi gani,wamefikia kipindi gani alafu TCU ihakiki ufaulu wa mwanafunzi mpaka alipoishia ili TCU iweze kuchukua hizo alama na kufata vigezo vyetu ili kurasimisha taaluma zao walizokuwa wanasoma nje ya nchi na waweze kuendelea na masomo katika vyuo vya ndani.” amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu ambapo Mbunge wa iimbo la Hai mkoani Kilimanjaro Saashisha Mafuwe alitaka Serikali itoe kauli kuhusu Wanafunzi waliorudi nchini kutoka masomoni nje ya nchi kutokana na vita au janga la UVIKO 19.