Vijana watakiwa kuyaenzi maono ya Mwalimu Nyerere

0
175

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema, Serikali itaendelea kuyaenzi maono ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuendelea kudumisha amani, umoja na ushirikiano.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Amesema kama lilivyo lengo la kongamano hilo, ni muhimu kuwarithisha vijana wa Kitanzania fikra na falsafa za Baba wa Taifa.

“Aidha, nyote mtakubaliana nami kwamba yapo mambo mengi ambayo tungetamani vijana wetu wayafahamu kuhusu urithi aliotuachia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Pia amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuheshimu misingi ya dini zote na kuwataka Watanzania kuendelea kuheshimiana na kupendana ili kujenga Taifa lenye ustawi wa amani na upendo.

Katika kongamano hilo Waziri Mkuu Majaliwa alipata nafasi ya kuzindua mpango wa kurithisha watoto na vijana mazur aliyoyaasisi Baba wa Taifa na uzinduzi wa klabu za mazingira za Mwalimu Nyerere kwa shule za msingi na sekondari.