Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Vijana nchini kujikita zaidi katika kutafuta fursa za kazi badala ya fursa za ajira.
Rais ametoa wito huo wakati wa kilele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibari huko wilaya ya mkoani Kusini Pemba.
Amesema ni lazima Vijana wakatambua kuwa ajira ambazo zimekuwa zikitangazwa hazitoshi, hivyo ni lazima wakajielekeza katika kufanya kazi ambazo zitawaingizia kipato chao cha kila siku.
Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Vijana ndio nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote duniani, kwa hiyo ni lazima wakawa na maono ya namna watakavyoliinua Taifa lao.
Ametumia kilele hicho cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibari kusisitiza malezi mema kwa vijana, kundi ambalo ni nguvu kazi kubwa kwa Taifa.
Kaulimbiu ya matembezi hayo ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibari ni uchumi wa bluu ni fursa kubwa kwa Vijana.
Matembezi hayo yalizinduliwa tarehe tatu mwezi huu na kushirikisha watembeaji 700 waliotembea umbali wa kilomita 124.9 nchi nzima.