Vijana watakiwa kupima vinasaba wa selimundu (sickle cell)

0
503

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewashauri vijana nchini kupima afya zao ili kufahamu kama wana vinasaba vya ugonjwa waSelimundu (sickle cell) ama la, ili waweze kutengeneza familia bora.

Waziri ametoa ushauri huo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Selimundu Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam.

Juni 19 kila mwaka, Tanzania imekuwa ikiungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha Siku ya Selimundu. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu hapa nchini ni Huduma Bora kwa Kila Mhitaji, Chukua Hatua Panua Wigo.

Ugonjwa wa Selimundu ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza yanayosababisha vifo vya watu wengi.