Vijana jiwekeeni malengo

0
229

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana wa Kitanzania wahakikishe wanajiwekea malengo ya kusoma kwa bidii ili kupata maarifa yatakayolisaidia Taifa kupata maendeleo.
 
Pia, Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Elimu kufanya mapitio ya sera ili kuifanya sekta hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi
 
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo alipokagua ujenzi wa madarasa ya shule za Sekondari za Gehandu na Nowu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
 
Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali kwa upande wake imejipanga ipasavyo na itaendelea kuweka mazingira bora ya kujifunza na kufundishia ili kuwawezesha kufikia malengo yao.
 
Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.
 
Pia, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote ziweke mpango wa ujenzi wa mabweni kupitia mapato yao ya ndani ili wanafunzi wakae shuleni na kupata muda wa kutosha wa kujisomea.
 
Waziri Mkuu pia amewakumbusha watumishi wa umma kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kuwatumikia Watanzania na kutekeleza maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya CCM.