Vijana 100 kila Halmashauri kushiriki kilimo cha kisasa

0
190

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema kuwa mradi wa kuwawezesha Vijana kushiriki katika kilimo cha Kisasa unaosimamiwa na Serikali utakua endelevu na utatumika kama kielelezo cha kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza katika matangazo ya moja ya moja kupitia Televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutoka viwanja vya Mpilipili mkoani Lindi, Waziri Mhagama amesema kuwa, Serikali imeamua kutumia kilimo cha Kisasa (Green House) kuwawezesha Vijana kushiriki katika kulima, kuongeza thamani na kutafuta masoko ya bidhaa za kilimo hapa nchini.

Amesema kuwa, kwa sasa Vijana 100 kutoka katika kila Halmashauri wamepewa mafunzo ya kutengeneza Green house, kutafuta masoko na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo ili kuongeza ufanisi katika mazao wanayolima.

Waziri Mhagama ameongeza kuwa, mradi huo umeanza mwaka 2018 na kuanzia mwaka 2020 Mwenge wa Uhuru utapita kukagua miradi hiyo katika kila Halmashauri nchini.