Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Deus Seif pamoja na Mwekahazina wa chama hicho Abubakari Allawi, wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yao vibaya kwa kuchepusha shilingi milioni 13.9 mali ya CWT.
Akitoa Hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Richard Kabate amesema, mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao na kila mmoja atatumikia kifungo cha miezi sita jela.
Mbali na adhabu hiyo mshtakiwa kwa kwanza ambaye ni Seif atakapomaliza kutumikia kifungo chake atatakiwa kuilipa CWT fidia zaidi ya shilingi milioni 7.5 na mshtakiwa wa pili ambaye ni Allawi atakapomaliza kutumikia kifungo chake atatakiwa kuilipa CWT shilingi milioni 6.2.
Awali jopo la mawakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambanna na Rushwa Nchini (TAKUKURU) liliiomba mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa adhabu kali kwa washtakiwa hao.