Vifo vya mama na mtoto bado tatizo

0
180

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angellah Kairuki amesema, bado kuna tatizo la vifo vya mama na mtoto nchini hivyo Serikali inaendelea na jitihada za kukabiliana na tatizo hilo.

Waziri Kairuki amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa makabidhiano ya jengo la upasuaji, wodi ya wazazi, vifaa vya huduma za dharura za afya ya uzazi na mtoto na gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Dabalo, Chamwino.

Majengo na vifaa hivyo ni msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kwa ushirikiano na Serikali ya Denmark na gharama ya yake ni zaidi ya shilingi Milioni 615.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Mark Bryan Screiner amesema, shirika hilo kwa kushirikiana na Denmark wameanzisha mradi wa kusaidia mafunzo ya kitaalamu kwa wataalam wa afya zaidi ya 600 katika mikoa ya Dodoma, Simiyu pamoja na Zanzibar.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uwezo kwa wataalam hao katika kutoa huduma, ili waweze kutoa huduma bora za uzazi.