Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na mjadala mkubwa kuhusu nafasi ya tiba asili katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona, ambapo baadhi wamekuwa wakisema ni tiba sahihi na salama huku kundi jingine likipinga.
Kufuatia mvutano huo, TBC imezungumza na Dkt. Joseph Otieno ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Dawa Asili kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Msikilize Dkt. Otieno hapa chini akielezea namna dawa hizo zinavyofanya kazi: