Vichanga walazwe nje

0
159
Close-up of an adorable little African baby reaching out while lying in an infant safety seat/carrier

Watoto wachanga duniani kote wanahitaji uangalizi na ulinzi wa karibu sana, ingawa kulingana na tamaduni mbalimbali malezi hutofautiana.

Baadhi ya nchi kama Finland, Denmark, Norway na hata Sweden watoto wachanga huachwa walale nje ya nyumba, duka au mgahawa kwenye baridi kali huku wazazi wakiwa ndani.

Japo wengine wanaweza kuona hii kama ukatili.

Wenyewe wanasema huu ni utamaduni wao na inaaminika kusaidia upumuaji wa mtoto, kuimarisha kinga mwili, kumfanya mtoto awe na mpangilio mzuri wa kulala na kumfanya ajitegemee zaidi.

Kwa mujibu wa ukurasa wa ITK unaeleza kuwa watoto huvalishwa na kufunikwa vizuri kisha kuwekwa kwenye kikapu chao na wakati mwingine hufunikwa kwa koti la mvua ili kuzuia uchafu kutoka nje usiwafikie.

Huku wakazi wanasema watoto hawaibwi, hivyo utamkuta mwanao pale ulipomwacha.