Uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha

0
152

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Leo anazindua Mpango Mkakati wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha wa mwaka 2023 – 2028, uzinduzi unaofanyika Dar es Salaam.

Huduma Jumuishi za Kifedha ni upatikanaji na matumizi endelevu ya bidhaa na huduma mbalimbali rasmi za fedha zenye ubora wa hali ya juu na gharama nafuu kwa mtu binafsi au biashara, ili kuboresha ustawi wa fedha na hadhi ya maisha.

Mkakati wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha wa mwaka 2023 – 2028 ni mkakati wa tatu kutekelezwa chini ya Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za Fedha.