Uzinduzi wa Kitabu cha Kiswahili na Teknolojia

0
168

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amezindua kitabu cha Kiswahili kilichoandikwa na Kaimu Mkuu wa Vipindi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Victor Elia.

Kitabu hicho kilichozinduliwa mkoani Arusha wakati wa Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani, kinazungumzia ukuaji wa kiswahili na teknolojia katika vyombo vya habari.