UWT yawataka Wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi

0
110

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umetoa wito kwa Wanawake nchini kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2025.

Akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha ziara ya viongozi wa UWT Taifa mkoani Njombe, Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatoa nafasi sawa kwa watu wote kugombea uongozi, hivyo amewahimiza Wanawake ambao ni Wanachama wa chama hicho wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi hizo.

Ziara ya viongozi wa UWT Taifa mkoani Njombe ilikuwa na lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.