Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Aretas Lyimo amesema, mradi wa kuendeleza bandari ya Dar es Salaam baada ya uwekezaji kufanyika, utasaidia kufanikisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Kamishna Jenerali Lyimo alikuwa akizungumza katika maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya duniani yaliyofanyika mkoani Arusha, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
“Sisi tunaona na kutambua kazi yako kubwa unayoendelea kuifanya katika kuiletea nchi yetu maendeleo hasa katika kipindi hiki cha changamoto za kichumi wa kidunia ambapo Serikali inaendela kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati nchi nzima ikiwemo ujenzi wa miundombinu mikubwa ya barabara na ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere. Halikadhalika ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uwekezaji na katika miundombinu ya mawasiliano na uchukuzi ikiwemo reli ya kisasa ya SGR na bandari ya Dar es Salaam ni hatua inayostahili pongezi”.
“Usimikaji wa mitambo ya kisasa ya utambuzi katika maeneo hayo husasani bandari ya Dar es Salaam baada ya uwekezaji utasaidia kudhibiti bidhaa haramu zikiwemo dawa za kulevya na kemikali bashirifu kuingia hapa nchini.“ Ame