Uwanja wa ndege Iringa wapata mashine

0
1015

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) imetoa mashine ya kielektroniki kwa ajili ya ukaguzi wa mizigo na abiria itakayotumika kwa abiria wanaotumia uwanja wa ndege wa Iringa.

Mashine hiyo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 300 imetolewa na TAA kufuatia ombi la mkuu wa mkoa wa Iringa,- Ally Hapi ikiwa ni mkakati wa mkoa huo wa kuboresha uwanja huo wa ndege ili kuwezesha ndege za Shirika la Ndege Nchini (ATCL) kutua na hivyo kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji.

Meneja wa uwanja wa Ndege wa Iringa, – Hanna Kibopile amesema kuwa kuwepo kwa mashine hiyo ya ukaguzi wa mizigo na abiria ni mwendelezo wa maboresho ya huduma za uwanja huo ambao upo katika ukarabati mdogo unaohusisha njia ya kuruka na kutua ndege, majengo ya abiria na ofisi mbalimbali.

Kibopile ameongeza kuwa mashine hiyo ya ukaguzi itaongeza usalama, tofauti na ilivyokua awali ambapo walikua wanakagua mizigo kwa kutumia mikono.