UVCCM kumpata mwenyekiti na makamu

0
65

Mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), unaendelea hivi sasa mkoani Dodoma.

Pamoja na mambo mengine mkutano huo unawachagua Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Wajumbe watatu wa halmashauri Kuu NEC kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar na Wajumbe wa Baraza Kuu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Mkutano huo ambao ni maalum kwa ajili ya uchaguzi, unasimamiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.

Wakati UVCCM ikifanya uchaguzi huo, Chama Cha Mapinduzi kimesisitiza kuwa ukomo wa umri kwa mwanachama anayegombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Umoja huo ni miaka 35.