UVCCM Kigoma yawataka Watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya corona

0
178

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kigoma, umetoa wito kwa Watanzania wote kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya kuhusu namna ya kujikinga na virusi vya corona.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kigoma, Katibu wa Hamasa na Chipukizi kutoka UVCCM mkoani humo Masanja Machai ametaka suala la homa ya corona lisichukuliwe kisiasa na badala yake wanasiasa washirikiane na serikali kupambana na homa hiyo.

Aidha UVCCM mkoani Kigoma imeipongeza serikali kwa hatua mbalimbali inazoendelea kuchukua katika kuzuia kuenea kwa virusi vya corona nchini.