Rais John Magufuli amemteua Dkt Buruhani Nyenzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Dkt Nyenzi anashika wadhifa huo kwa kipindi cha Pili.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt Makame Omar Makame kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA.
Dkt Makame ni Mhadhiri Mwandamizi wa Jiografia katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa, uteuzi wa viongozi hao umeanza Novemba 18 mwaka.
