Uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Naibu Katibu Mkuu, DC na DED

0
331

Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo amemteua Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo Kabunduguru alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu na anachukua nafasi ya Hussein Katanga ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Rais Magufuli pia amemteua Godfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Mipango wa wizara ya Sheria na Katiba.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu imeeleza kuwa Hashim Komba ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.

Kabla ya uteuzi huo Komba alikua Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa na anachukua nafasi ya Rukia Muwango ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Mwingine aliyeteuliwa ni Hassan Rungwa anayekua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kuchukua nafasi ya Bakari Mohammed Bakari ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.