Uteuzi wa mkurugenzi mkuu MSD watenguliwa

0
518

Rais John Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Dkt Gabriel Mhidize kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa – MSD.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa, uteuzi wa Brigedia Jenerali Dkt Mhidize unaanza mara moja.

Kabla ya uteuzi huo, Brigedia Jenerali  Dkt Mhidize alikuwa Mkuu wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar es salaam.

Brigedia Jenerali Dkt Mhidize anachukua nafasi ya Laurean Bwanakunu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.