Uteuzi wa Diwani Athumani watenguliwa

0
166

Rais Samia Suluhu ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani Msuya.

Diwani aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu Januari 3, 2023 katika mabadiliko madogo yaliyofanyika Serikalini.

Wakati huo huo, Rais amemteua Mululi Mahendeka kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.