Uteuzi wa DC na DED Malinyi watenguliwa

0
165

Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, -Majura Kasika na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Mussa Mnyeti.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu imeonyesha kuwa, uteuzi wa viongozi hao umetenguliwa kuanzia hii leo.

Uteuzi wa viongozi watakaojaza nafasi hizo katika wilaya hiyo ya Malinyi utafanyika baadaye.