Uteuzi uliofanywa na Dkt Magufuli

0
329

Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, ambapo amemteua Profesa Blasius Nyichomba kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Profesa Nyichomba ni Profesa Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwingine aliyeteuliwa na Rais Magufuli ni Dkt Rosemarie Mwaipopo anayekua Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa, kwa sasa Dkt Mwaipopo ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Profesa Longinus Rutasitara, yeye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Rais Magufuli pia amewateua Rhoda Ngamilanga na Devotha Kamuzora kuwa Makamu Wenyeviti wa Baraza la Rufani za Kodi.

Profesa Yunus Mgaya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), ambapo anashika wadhifa huo kwa kipindi kingine cha miaka miwili.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza hii leo.