Takribani watu elfu 40 wanaelezwa kuugua saratani mbalimbali huku asilimia 7 kati ya hao wakikutwa na tatizo la saratani ya damu hivyo wataalamu wa afya kutakiwa kushirikiana na Serikali kuelimisha jamii kuona umuhimu wa kupima afya zao.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya afya Profesa Abel Makubi mara baaada ya kuzindua kongamano la utafiti wa Saratani ya damu iliyofanyika katika Chuo Kikuu Shirikishi Cha Afya ya Sayansi Cha Muhimbili (MUHAS)
Profesa Makubi amebainisha kuwa kufanyika kwa kongamano hilo utasaidia wataalam kuja na mawazo mbadala yatakayosaidia kuokoa maisha ya Watanzania wengi wanaougua tatizo la saratani ya damu bila kujua.
“Jamii bado inahitaji kuelimishwa zaidi juu ya saratani ya damu ili waweze kutambua dalili zake mapema na tatizo kutafutiwa ufumbuzi kwa wakati”, Amesisitiza Profesa Makubi.
Baadhi ya watu waliowahi kukutwa na tatizo la saratani ya damu wameushauri jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya zao ili wanapojigundua waweze kusaidiwa haraka iwezekanavyo kuondokana na changamoto hiyo ya saratani.