Usikilizwaji wa mashauri mahakamani waongezeka

0
178

 
Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene amesema Serikali imedhamiria kuendelea kufanya maboresho kwenye sekta ya sheria.  ili kuwarahisishia Wananchi kupata huduma stahiki na kwa wakati unaofaa.
 
Waziri Simbachawene ametoa kauli mkoani Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari ambapo alikuwa akielezea mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya sheria katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.
 
Amesema kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika kwenye sekta ya sheria hasa suala la utoaji haki, usikilizwaji wa mashauri mahakamani umeongezeka.
 
Kwa mujibu wa Waziri Simbachawene, katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi mwaka 2021 hadi Februari mwaka huu. jumla ya mashauri 1,391 yalishughulikiwa na ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambapo kati ya hayo ya madai ni 1,274 na ya usuluhishi 117.
 
Kuhusu usajili wa Taasisi za msaada wa kisheria, Waziri Simbachawene amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi  Machi mwaka  2021 hadi mwezi  Februari  mwaka huu,  taasisi 170 za aina hiyo zimesajiliwa,  hali iliyosadia kupunguza adha kwa Wananchi  kutembea umbali mrefu kufuata huduma za kisheria.