Usikilizwaji Rufaa dhidi ya Sabaya kuendelea Januari 17

0
128

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imesema Januari 17, 2023 itaendelea na usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) katika kesi ya uhujumu uchumi, ambapo anapinga hukumu iliyomwachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Katika rufaa hiyo, DPP anapinga hukumu ya Juni 10, 2022 iliyotolewa na Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliyowaachia huru Ole Sabaya, Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.