Ushirikiano wa Tanzania na jimbo la Fujian kuendelezwa

0
2018

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi -CCM Dkt Bashiru Ally amemkabidhi zawadi ya kinyago Gavana wa jimbo la Fujian mjini Fuzhou nchini China kama alama ya urafiki wa jimbo hilo na Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi kinyago hicho, Dkt Bashiru amemuhakikishia Gavana huyo wa jimbo la Fujian kuulinda undugu huo ikiwa ni pamoja kutilia mkazo mambo matatu ya kuelekea maendeleo.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni fursa za kibiashara kati ya Tanzania na jimbo la Fujian, utalii na utafiti wa kitaalam.